Back

Wacheza gofu mashuhuri 81 kushiriki mashindano ya Serengeti

JUMLA ya wachezaji mashuhuri 81 wa gofu kutoka Tanzania Kenya, Uganda, Rwanda na Malawi wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya mchezo wa gofu yanayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia leo Oktoba 15 – 17, 2026 katika uwanja wa gofu uliopo Fort Ikoma – Serengeti almaarufu “Serengeti National Park Golf Course”. Mashindano yatakayofanyika kwa siku 3 mfululizo kuelekea siku ya uzinduzi wa uwanja huo Oktoba 18, 2026.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Massana Mwishawa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa uwanja huo.

Kamishna Mwishawa alielezea kuwa mradi huo wa kimkakati umekamilika wa asilimia 100 huku ukilenga kukuza utalii wa michezo, kuongeza thamani ya vivutio vya utalii Tanzania, kufungua fursa za kiuchumi kwa jamii kupitia ajira, biashara na kuongeza vionjo vipya kwa mtalii ili aongeze siku za kukaa hifadhini na kupata uzoefu mbashara.

TANAPA inatarajia kuzindua rasmi huo (Serengeti National Park Golf Course) Oktoba 18, 2026 katika eneo la Fort Ikoma lililopo pembezoni kidogo mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Uwanja huo wenye mashimo 18 na par 72 utazinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt. Samia Suluhu Hassan.

The full article is being collected. Available text is shown for now.

Back
Share this story

Get the daily newsletter →

Ask globalread.info

AI news & website helper
What would you like to explore?

I can find stories, explain headlines, or help you use globalread.info.

AI can make mistakes. Check the linked sources. Questions are sent to OpenAI.