RAIS SAMIA ATEUA MABOSI WAPYA TTB NA TBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili wa taasisi za Serikali, akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Taarifa iliyotolewa Oktoba 13, 2026, na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu. na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dkt. Samia amemteua Dkt. Thereza Israel Mugobi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mugobi alikuwa akikaimu nafasi hiyo na sasa amethibitishwa rasmi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTB.
Aidha, Rais Samia amemteua Bw. Said Rajabu Mndeme kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mndeme alikuwa Mkurugenzi wa Milki katika TBA.
Bw. Mndeme anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Bw. Daud Kondoro, ambaye amemaliza muda wake.
Related Stories
TFRA YAWATAKA WAKULIMA KUPIMA UDONGO KABLA YA KUTUMIA MBOLEA
Wakulima wametakiwa kuzingatia upimaji wa afya ya udongo kabla ya kutumia mbolea ili kubaini virutubisho vinavyohitajika na kuchagua aina inayofaa kwa mazao yao, hatua…