Back

Vurugu katika kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha Raila

Story illustration

HAFLA ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga ilikumbwa na vurugu katika Kituo cha Utamaduni cha Migwena, Bondo, Kaunti ya Siaya, huku makundi hasimu ya kisiasa yakizozania urithi wake na mwelekeo wa chama hicho.

Vijana waliojihusisha na wanasiasa tofauti walifurika kwenye hema la wageni mashuhuri, wakitatiza shughuli na kufanya iwe vigumu kwa viongozi kufuatilia ratiba ya hafla hiyo.

Maombi yaliyoongozwa na Kanisa la Kianglikana nchini yalianza mwendo wa saa tano asubuhi, yakifuatiwa na hotuba za wanafamilia na burudani za muziki.

Hata hivyo, juhudi za msimamizi wa hafla kuwatawanya vijana hao hazikufaulu, hali iliyolazimu mjane wa Raila, Mama Ida Odinga, pamoja na watoto wao Raila Junior, Rosemary na Winnie, kuhamia hema nyingine.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya baadhi ya vijana kuanza kurusha mawe kuelekea hema la wageni mashuhuri. Maafisa wa usalama waliokuwa wakilinda viongozi walitumia viti vya plastiki kuwakinga huku waliohudhuria wakitafuta mahali pa kujisitiri. Baadhi ya watu waliripotiwa kujeruhiwa.

Vurugu hizo zilitokea huku kukiwa na mvutano kati ya wanasiasa wanaounga mkono mrengo wa Linda Mwananchi na wale wanaounga mkono ushirikiano wa ODM na serikali ya Rais William Ruto.

Licha ya hali hiyo, hafla iliendelea huku familia ikitoa heshima kwa Raila, aliyefariki mwaka mmoja uliopita.

Mama Ida aliwaomba vijana kuwa watulivu na kueleza kuwa mwaka uliopita ulikuwa mgumu kwa familia, ambayo pia ilimpoteza dada yake Raila ndani ya siku 40 baada ya kifo chake.

Alisema bado wanaomboleza na akawashukuru wakazi wa Bondo, Kisumu na Wakenya wengine kwa kuendelea kuwafariji.

Mama Ida pia alikumbuka jinsi alivyokabidhi mumewe wananchi aendelee na safari yake ya kisiasa, akisema alitamani angerudi nyumbani akiwa hai.

Aliwataka viongozi na wazee kuwaelekeza vijana kwa upendo na subira, huku akiwahimiza vijana kuwaheshimu wazee.

Vurugu hizo ziliangazia mgawanyiko unaozidi kujitokeza ndani ya ODM kuhusu jinsi ya kuendeleza siasa za Raila na msimamo wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

The full article is being collected. Available text is shown for now.

Back
Share this story

Get the daily newsletter →

Ask globalread.info

AI news & website helper
What would you like to explore?

I can find stories, explain headlines, or help you use globalread.info.

AI can make mistakes. Check the linked sources. Questions are sent to OpenAI.